BAADA ya kusumbuliwa na presha ya kushuka mara kwa mara, iliyosababishwa na stress za kutendwa na wanaume, hatimaye msanii wa filamu Bongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ ametuliza mzuka baada ya kumpata mpenzi mpya anayeishi ughaibuni.
Msanii wa filamu Bongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ akipozi.
Akipiga stori na gazeti
hili majuzi, Amanda alisema ni kweli kwa sasa ana furaha baada ya
kumpata mwanaume anayeamini ni muaminifu baada ya watu wake wa zamani
kumtenda na hivyo kujikuta akiwa katika hali mbaya.
“Kwa kweli hivi sasa nipo
poa sana. Mpenzi wangu anaishi Europe na siwezi kumtaja jina wala
uraia wake kwa sasa, kwa sababu naogopa kuibiwa, pia nataka nifanye
sapraizi kwa mashabiki na marafiki zangu, siku ikifika ya utambulisho
watamuona,”alisema.