MAMA mmoja mjane, Mwajuma Hamisi Lissu (42) ameteketea kwa moto baada ya nyumba aliyokuwa amelala eneo la Kibamba Hondogo A maarufu Miti Mirefu jijini Dar es Salaam, kulipuliwa kwa petroli usiku wa Agosti 24, mwaka huu.
Tukio hilo la kusikitisha
inadaiwa linahusishwa na ugomvi baada ya mama huyo kuachana na
ulokole na kujiunga tena katika dini yake ya zamani ya
Kiislamu.Akisimulia mazingira ya tukio hilo, mtoto wa pili wa mama huyo
ambaye hivi sasa ni marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Charity
Jikole alikuwa na haya ya kusema:
“Mama amelipuliwa na
petroli. Baada ya moto huo kulipuka chumbani tulikuta nyavu za kwenye
dirisha la chumba alicholala zimekatwa, tunaamini mlipuaji ndiye
aliyekata nyavu hizo na kupitishia petroli.
“Mauaji haya siyo ya bahati mbaya bali yanatokana na mkono wa mtu kwani hata moto ulipokuwa unawaka harufu ya petroli ilikuwepo eneo hilo.
“Mauaji haya siyo ya bahati mbaya bali yanatokana na mkono wa mtu kwani hata moto ulipokuwa unawaka harufu ya petroli ilikuwepo eneo hilo.
“Mkasa huu unatokana
na ukweli kuwa mama yangu awali alikuwa Muislamu lakini kutokana na
matatizo yake ya kiafya alishauriwa na baadhi ya watu kujiunga na
maombi katika makanisa ya kilokole ili awe anaombewa tatizo la presha. “Baada ya kushauriwa aliamua kujiunga na makanisa hayo ya kilokole akiamini kuwa angeweza kupona.
“Mama alikuwa ni mjane mwenye watoto watatu na baada ya kujiunga na walokole amekuwa akisali katika makanisa manne tofauti. “Sisi
kama familia tunawatuhumu walokole kwa sababu hata baada ya moto
huo, baadhi yao hawakuja kusaidia kuuzima wala kutoa maji.
“Kwa kweli tulishangazwa na kitendo hicho na kuwaona ni watu wabaya sana kwetu.”
Hata hivyo, mtoto huyo
alisema kifo cha mama yake kimekuja siku moja baada ya kufanyiwa
sherehe ya kutoka katika dini ya kilokole na kurudi kwenye Uislamu.
Mchungaji aliyetajwa kwa
jina la George Said ambaye anawaongoza walokole wa eneo hilo,
alipohojiwa na waandishi wetu alikiri kusikia tuhuma hizo. “Hata
mimi nimesikia tuhuma hizo lakini si za kweli hata kidogo na mpaka
sasa sijahojiwa na mtu yeyote au hata polisi kuhusiana na tatizo hilo,” alisema mchungaji huyo.

