Advertisement

Responsive Advertisement

CHUCHU HANS AWACHARUKIA WOTE WASIO PENDA MAPENZI YAKE NA MWIGIZAJI RAY KIGOSI

Stori: Imelda Mtema

MALOVEE! Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans, amewashukia watu wanaoiponda ‘kapo’ yake na mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na kusema hata iweje, mambo yao yatakwenda kama walivyopanga.

Chuchu alisema katika maisha ya mwanadamu kama Mungu amepanga kitu siku zote kitatimia hivyo anaamini wanaopinga uhusiano wao kwa maneno ya chinichini na kwenye mitandao ya kijamii ni maadui lakini hawatashinda.

Najua kabisa nina maadui wengi sana lakini naamini Mungu atasimama wanaiponda sana ‘kapo’ yetu lakini Mungu akipanga kitu siku zote lazima kitatimia  hakuna ubishi,” alisema Chuchu.


Kabla ya kuwa na uhusiano na Ray, Chuchu aliwahi kuolewa na mtangazaji Frank Mtao ambaye inasemekana wameshamwagana.
GPL