Toka
namba mpya za magari zianze kutumika nchini Tanzania tulizoea kuona
namba hizo zikifanana na zile za pikipiki, yani hakukuwa na tofauti kati
ya namba za pikipiki na za magari. Taarifa mpya ya TRA iliyoandikwa na gazeti la Uhuru imesema kuanzia
October 2014 mamlaka hii ya mapato itaanza kutoa namba mpya za pikipiki
ambazo zitakuwa tofauti na namba za magari. Namba hizo mpya zitakua kwenye mfano huu MCM 101 AAA badala ya T101AAA