Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania Ernest Mangu
Kufuatia
msako mkali uliofanywa jana na jeshi la polisi nchini katika mkoa wa
Geita eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe wamefanikiwa kumkamata mtu
mmoja waliyekuwa wakimhisi kuwa ni jambazi ambaye amekutwa akiwa ameketi
juu ya mti na akiwa ameshikilia bomu.
Majambazi
hayo yalivamia kituo cha polisi na kuua askari polisi wawili na habari
zinadai kuwa askari aliyejulikana kwa jina la David alifariki dunia
baada ya kufikishwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Mtu
huyo ambaye hakufahamika jina alikutwa juu ya mti majira ya jioni
wakati msako mkali wa jeshi la polisi ukiendelea katika eneo hilo huku
wakikuta bunduki saba aina ya SMG zikiwa zimewekwa kwenye tanuru la
kuchomea matofali.