Wakiongea kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wananchi wa kata hiyo kwa sharti la kutotaka kutajwa majina yao walisema
diwani huyo amekuwa ni kero kwa watu kwani amekuwa akiwatapeli watu kwa
kuwapatia tiba za uongo na kuwachonganisha watu bila kuona kuwa yeye ni
kiongozi.
Walisema
diwani huyo amekuwa akiwapigia ramli chonganishi watu wanaokwenda kwake
kwa ajili ya kupata tiba ya kienyeji hivyo kuwaomba wanaohusika
kuchukua hatua dhidi ya diwani huyo.
"Jamani
huyu diwani wa CCM ni tapeli anawachonganisha wananchi mpaka wanafika
hatua ya kuuana ,kwanza si mganga bali ni tapeli ni mganga gani ufike
unaambiwa kiasi kikubwa cha fedha ",walisema.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Juma Choba alikiri kukamatwa kwa diwani wake lakini akasema kuwa alikamatwa kwa tuhuma za kuwaosha wakataji wa mapanga katika kata hiyo.
Hata
hivyo alisema hajui kama ni kweli anafanya kazi hiyo kwani hajawahi
kuona ila anasikia kutoka kwa wananchi kuwa diwani wake anawapigia ramli
chonganishi.
"Mimi
nasikia kama wewe unavyosikia lakini sijawai kumuona ila amekamatwa
yuko Polisi Wilayani inawezekana ni kweli kwa kweli siwezi
kukataa",alisema Mtendaji huyo.
Akizungumza na malunde1 blog iliyotaka kujua zaidi kuhusu tuhuma hizo za kukamatwa kwake na kupiga ramli chonganishi , diwani Mawazo alisema kuwa yeye hana lolote la kujibu juu ya hilo.
Jeshi la polisi Mkoani Geita limethibitisha kukamatwa kwa diwani Mawazo na uchunguzi unaendelea kubaini ukweli wa tukio hilo.
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita