Wananchi
wilayani Geita Mkoani Geita wamemuomba mkuu wa jeshi la polisi nchini
(IGP) Ernest Mangu(PICHANI) kumrudisha aliyekuwa kamanda wa wa mkoa huo
Leonad Paulo aliyehamishiwa mkoa wa Morogoro hivi karibuni.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti wakazi wa mkoa huo wametoa kilio hicho kutokana na
kukithiri kwa mauaji yanayosababishwa na majambazi ambao wamefanya
wakazi wa mji huo kukosa amani na kushindwa kufanya kazi zao za kila
siku kwa kuogopa kuvamiwa.
Wamesema
katika kipindi yupo kamanda Paulo majambazi waliisha na mauaji ya
vikongwe yalipungua kwa kasi lakini kwa sasa vikongwe wanazidi kukatwa
na kuuawa huku majambazi wakizidi kumaliza maisha ya ndugu na jamaa na
sasa wameanza kuua askari polisi.
Wamesema matukio makubwa ambayo yametokea kwa kipindi cha muda
mfupi tangu kamanda Paulo aondoke ni lile la majambazi kuwavamia
wafanya bishara wawili na kumuua mmoja wao Gozibati Warwa aliyeuawa
mchana kweupe saa kumi na moja jioni na kuchukua pesa na bastola na
kutokomea na kukamatwa mda mfupi.
Mmoja wa mwananchi hao Masanja Juma kutoka Katoro wilayani Geita amelitaja tukio la pili kuwa ni lile la majmbazi kuvamia kituo cha polisi cha Bukombe na kuua askari wawili ambao ni PC Dastan Kimati(25) na Horia Mwandija(30) na kujeruwi wawili, Mohamed Hassan(25 na Devid Ngutama(44) ambapo pia walibeba bunduki na mabomu pamoja na risasi na kutokomea kusikojulina
Amesema japokuwa bunduki inasemekana zimekamatwa lakini wananchi bado wana hofu kubwa.
"Mimi
kama mwananchi wa Geita namuomba (IGP) amrudishe Kamanda Paulo kwani
alikuwa anajaribu kutumia mda mwingi kuongea na watu wa aina zote,ofisi
yake ilikuwa wazi kila wakati kwa watu wote, ndio maana na
alipopelekewa tatizo alifuatilia mara moja na kutatua" amesema Juma.
Hata
hivyo kufuatia matukio ya kuendelea kuuawa kwa watu yamezidi kuwafanya
wakazi wa mji huo kutofanya kazi zo kwa uhuru hivyo wamemwomba IGP
kutenga kanda maalumu katika mkoa wa Geita huenda ikapunguza mauaji.