Mwalimu
wa kanisa Katoliki, Magharibi ya Kenya alijikuta taabani baada ya
kutekwa nyara na majambazi waliomtesa pamoja na kumpiga msumari kwenye
mti msituni, umbali wa kilomita miambili kutoka nyumbani kwake.
Peter Asutsa alikaa msituni kwa saa 16 mkono wake ukiwa unaning'inia kwenye mti kabla ya kuokolewa na polisi.
Inaarifiwa
Peter alipigwa msumari kwenye kwenye mkono wake mmoja baada ya
majambazi hao kukosa kumpata na pesa zaidi walizokuwa wakitaka.
Inaarifiwa Asutsa aliizima simu yake na kuificha ndani ya nguo zake za ndani ambapo majambazi hao wasingeweza kuipata.
Baada ya majambazi hao kumtelekeza, alimpigia simu mkewe ambaye aliwaarifu polisi waliokuja kumuokoa.
Masaibu
ya Asutsa yalianza pale alipokwenda dukani kumnunulia mkewe mgonjwa
dawa katika duka la dawa mjini Kitale Magharibi ya Kenya.
Abiria
mmoja aliyekuwa ndani ya gari alimokuwa anasafiria Asutsa aliamrisha
dereva kusimamisha gari. Kisha akawafungia ndani akiwa na abiria wengine
wawili.
Alitekwa
nyara na majambazi waliofika katika sehemu hiyo kwa gari jingine na
kumuingiza ndani ya gari hilo na hapo ndipo alipogundua kuwa alikuwa
ametekwa nyara.
Walimpora dola 24 na kumtaka asalimu simu yake , lakini akataa.
Baadaye
walimpeleka ndani ya msitu na kumpigia msumari mtini kupitia kwenye
mkono wake mmoja na kumuacha ndani ya msitu wa Kaptagat.
Alilazimika kuwatisha na kuwafukuza Fisi na Mbweha waliokuwa wakitishia kumvamia usiku.
Aliambia BBC kuwa alihisi maumivu makali.
via>>BBC