MAMA
mmoja (jina lake linahifadhiwa kwasasa) amefariki baada ya wahudumu wa
zahanati
moja ya mjini Iringa kujaribu kumtoa mimba bila mafanikio.
Tukio
hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano ya wiki iliyopita katika zahanati
hiyo
iliyopo mjini hapa.
Baada
ya taarifa hizo kuvuja, habari zilizoufikia mtandao huu zinaonesha
kwamba
Polisi walitia timu katika kituo hicho cha kutolea huduma jana na
kuwakamata
wahudumu wote waliokuwepo zamu katika Zahanati hiyo binafsi.
Wakati
watoa huduma wakiachwa bila msaaada wowote katika selo ya Polisi Kati
mjini
Iringa,ndugu wa mkurugenzi huyo walifika na kumtoa mkurugenzi huyo baada
ya
kukamilisha taratibu za dhamana.
Mpashaji
wetu amesema kabla ya kifo chake mama huyo alifika kituoni hapo akihisi
ana
ujauzito alioupata bila ridhaa yake.
Ili
asitishe uhai wa kiumbe kilichoanza kuumbwa katika tumbo lake, mama huyo
aliahidi
kutoa sh 70,000 kwa mmoja wa watoa huduma wa zahanati hiyo ili atolewe
mimba
hiyo.
Kwa
kuwa hakuwa na ujuzi, mtoa huduma huyo anadaiwa kutumia vifaa
visivyotakiwa
kutoa mimba hiyo hali iliyomsababishia mama huyo maumivu makali.
Hali
ya mama huyo ilizidi kuwa mbaya baada ya kufika nyumbani kwake maeneo ya
frelimo mjini Iringa.
Pamoja
na ndugu wa mama huyo akiwemo mwanaume anayesadikika kuwa ni mumewe
kumrudisha mama
huyo katika zahanati hiyo, watoa huduma waliokuwepo zamu ya jioni ya
siku hiyo
aliyotolewa mimba, walihofia kumpokea kwa kile kinachoelezwa alikuwa
katika
hali mbaya.
Badala
ya kumpeleka hospitali ya mkoa, ndugu hao walirudi na mama huyo nyumbani
na
taarifa zinaonesha kwamba alifariki saa moja baadaye.
Bada
ya Polisi kunasa taarifa hizo walizuia mwili wa mama huyo usizikwe mpaka
ulipofanyiwa uchunguzi na kubainika alikufa baada ya kukatwakatwa nyama
za
mlango wa uzazi wakati shughuli ya utoaji mimba ikiendelea.
0 Comments