HUKU
wadau mbalimbali wa Habari wakiendelea kulaani vikali kitendo
cha Jeshi la polisi kuwapiga wanahabari wakati wakiwa kazini katika
tukio lilitokea Mwishoni mwa wiki iliyopita Makao makuu ya Jeshi la
polisi nchini wakati Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Freeman Mbowe
akijisalimisha polisi,
Katika hali ya kushangaza Serikali imesema haina taarifa juu ya kupigwa kwa mwandishi yoyote wa habari.
Kauli hiyo ya Kushangaza
imetolewa leo jijini Dar Es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo, Asah Mwambene alipokuwa anatembelea miradi ya maendeleo ya
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mbagala Jijini Dar Es Salaam.
Tanesco imetimiza miaka 50 toka ianze kutoa huduma ya usambazaji nishati kwa wananchi nchini kote.
Tanesco imetimiza miaka 50 toka ianze kutoa huduma ya usambazaji nishati kwa wananchi nchini kote.
Mmoja
wa waandishi wa habari aliyekuwepo katika ziara hiyo (toka gazeti la
mwananchi) alitaka kupata kauli kutoa kwa Mkurugenzi huyo kuhusiana na
tukio lililofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya wanahabari waliokuwepo
kazini wakati Mbowe akifika Polisi.
Mwambene
ambaye pia ni Msemaji wa Serikali alisema, hana taarifa za kupigwa kwa
waandishi wa habari bali katika tukio hilo lililohusisha wanachama wa
Chadema kukusanyika makao makuu ya jeshi hilo wakati kiongozi wao
akijisalimisha.
“Serikali haina taarifa
za kupigwa kwa waandishi, nakuomba tuzungumeze vitu vingine ”Alijibu
Mwambene.
Hata hivyo baadhi ya watu walisikika wakinong'ona wakisema; “tumemsikia mwandishi mmoja akilalamika sana kwenye vyombo vya Habari, ni Josephat Isango wa gazeti la
Tanzania Daima ambaye anaeleweka kabisa kwamba ni mwanachama wa chadema."
Mnong'onezaji huyo alisikika akisema Isango aliwahi kugombania Ubunge kupitia chama hicho.
Mnong'onezaji huyo alisikika akisema Isango aliwahi kugombania Ubunge kupitia chama hicho.
Kauli hiyo ya Mwambene
inatafsiriwa tofauti na wadau wa Masuala ya Habari kwani kuzungumza huku
kunazidisha maswali mengi kutokana na Idara ya habari maelezo ndio
inayowasimamia Waandishi pamoja na Magazeti.
Kwa
Upande wake, Josephati Isango amenukuliwa akithibitisha kuwa na nia ya
kumburuza mahakamani CP Chagonja, polisi watatu waliompiga pamoja na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
“Nawasiliana
na wanasheria wangu watatu jinsi ya kwenda mahakamani kuwashitaki
polisi watatu, Cp Chagonja na waziri mkuu ambaye mnakumbuka alishawhi
kutoa maagizo ya kupiga watu ovyo yanayotekelezwa na Polisi
hivisasa,”alisema Isango.
0 Comments