Advertisement

Responsive Advertisement

SAMATTA NA ULIMWENGU HAWAKWENDA NA STARS BURUNDI, WAISHIA KUFANYA MAZOEZI DAR NA KUREJEA TP MAZEMBE

Hawajakwenda; Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta hawajakwenda na taifa Stars Burundi
WASHAMBULIAJI Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu hawajaenda na Taifa Stars Burundi na badala yake wamerejea DRC kujiunga na klabu yao, TP Mazembe.
Sababu ya kurejea kwao Lubumbashi ni baada ya kukosa ndege ya moja kwa moja kutokea Bujumbura kwenda Kongo mara tu baada ya mechi, ili wawahi majukumu ya klabu yao.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika jitihada zake lilipata ndege ya kwenda Zambia ili wachezaji hao wakaondokee kwa basi mjini Ndola, kwa kuwa ni karibu na Lubumbashi, lakini hawakuwa tayari kutumia usafiri huo.
Kocha Mholanzi, Mart Nooij akaridhia nyota hao wawili warejee Kongo kuendelea na majukumu ya klabu yao baada ya jitihada zote kushindikana. Mazembe itacheza na FC MK kesho Uwanja wa Stade TP Mazembe mjini Lubumbashi, Ligi ya DRC na baada ya hapo, Septemba 20 itachea na ES Setif nchini Algeria katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Maana yake, Stars imeondoka jana na wachezaji 18 kwenda Bujumbura kwa ajili ya mchezo huo na wenyeji kesho.
Walioondoka ni makipa Mwadini Ally (Azam FC) na Deogratias Munishi 'Dida' (Yanga), mabeki 
Shomari Kapombe (Azam FC), Oscar Joshua (Yanga), Said Morad (Azam FC), Nadir Haroub 'Canavaro' (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Joram Mgeveke (Simba), Simon Msuva (Yanga), Erasto Nyoni (Azam FC), Himid Mao (Azam FC), Amri Kiemba (Simba), Haruna Chanongo (Simba), Salum Abubakar 'Sure Boy' (Azam FC), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Khamisi Mcha (Azam FC), Juma Luizio (Zesco United, Zambia) na Mrisho Ngassa (Yanga SC)
Tayari kocha Nooij aliwaacha mshambuliaji mwingine tegemeo, John Bocco 'Adebayor', beki Agrrey Morris na kipa Aishi Manula wote wa Azam FC, kwa sababu ya majeruhi.