Kwa kuguswa na tukio hili waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe ilibidi aahirishe ratiba zake nyingine na kulazimika kuja Musoma kuwatembelea majeruhi leo asubuhi kwenye hospitali ya mkoa pamoja na kwenda kwenye eneo la ajali kutazama.
Baada ya hapo Waziri Mwakyembe akaongea na millardayo.com na kueleza yafuatayo >> ‘Inabidi niwape pole Watanzania wote ambao wamepoteza ndugu jamaa na marafiki, taarifa za ajali nimezipata nikiwa Dodoma kwenye bunge maalum ikawa sasa nitafikaje haraka Musoma kwa hiyo ikabidi nitafute ndege leo asubuhi kuja hapa’
- Tunaanza na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku anamuona mwenzake na kusema mimi lazima anipishe’ – Dr. Mwakyembe
-
Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha
zao lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya
kupeleka abiria yaendeshwe na watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa
kila dereva kwamba amejiunga na hii mifuko ya akiba ya Wafanyakazi,
tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi’
-
Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe
tu ukipoteza gari ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu
binadamu…. bila comprehensive haendeshi mtu gari kuchukua abiria.
Kwa maelezo zaidi unaweza kumsikiliza Waziri Mwakyembe kwa kubonyeza play hapa chini