Ripota wa TZA (millardayo.com na AyoTV) Kenya Julius Kepkoich anatiririka kwamba Uhuru Kenyatta ametajwa kama rais anayejitokeza kwa njia ya kipekee toka Kenya ianze kutawaliwa akiwa pia ni rais wa kwanza kenya kumiliki kiti kilichowahi kukaliwa na baba yake.
Tangu kutwaa madaraka Kenyatta amekua akifanya mambo yasiyo ya kawaida kwa Rais yeyote hasa hapa Afrika yeye ametajwa kua anatumia sana mitandao ya kijamii kuwasiliana na watu, pia amewashangaza wengi kwa kutumia gari moja tu kwenye shughuli zake za kibinafsi.
Kingine alichotajwa nacho ni kujichanganya na raia wengine wa kawaida kwenye maisha ya kawaida kabisa hata kununua karanga kwenye foleni ya magari, kujivinjari ufukweni Mombasa na wakenya tu wa kawaida.
Wiki hii Rais Kenyatta anatufungia wiki kenya kwa picha za kipekee
alizopost akiwa na magwanda ya kijeshi juu chini, ikasababisha iwe ni
trend kwenye mitandao na kila mtu akaandika chakwake, mwingine military Swagg, ameamua kwenda somalia mwenyewe, the happiest Army officer na commander in chief na mengineo