Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Iraq na Syria (ISIS)
limetekeleza mauji mengine ya kutisha kwa kumkata kichwa mwandishi mwingine wa habari wa
Marekani.
Mwandishi huyo aliyetajwa kwa
jina la Steven Sotloff mwenye umri wa miaka 31 alitekwa na
wapiganaji hao mwezi August mwaka jana.Mwezi uliopita Sotloff alionekana
mwishoni katika picha za video
zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani
James Foley.
Katika video hiyo iliyopachikwa hapo chini, mwandishi huyu anaonekana kuuawa na mtu anayemruhusu kutoa semi yake ya mwisho.
Sotloff ambaye katika video hiyo amevalia magwanda ya rangi ya chungwa akiwa amepiga magoti anasikika akisema kuwa:
'Obama, your foreign policy of intervention in Iraq was supposed to be for preservation of American lives and interests, so why is it that I am paying the price of your interference with my life?.''
Mpiganaji mmoja wa kundi hilo akizungumza kwa kiingereza anamlaumu Rais Obama kwa kifo cha mwandishi habari huyo.
“I’m back, Obama, and I’m back because of your arrogant foreign policy towards the Islamic State..
“As your missiles continue to strike our people, our knife will continue to strike necks of your people,” anasikika akisema kabla ya kutekeleza kitendo hicho cha kikatali.
Muuaji huyu anasadikika kuwa ni yule yule aliyemchinja mwandishi wa kwanza mwezi uliopita.
“As your missiles continue to strike our people, our knife will continue to strike necks of your people,” anasikika akisema kabla ya kutekeleza kitendo hicho cha kikatali.
Muuaji huyu anasadikika kuwa ni yule yule aliyemchinja mwandishi wa kwanza mwezi uliopita.
Punde baada ya kukamilisha hotuba yake,muuaji huyo anaanza kumchinja Sotloff lakini video hiyo inazimwa .
Sekunde chache baadaye mateka mwingine raia wa Uingereza David Cawthorne Haines, anaonekana kabla ya ilani kutolewa
kuwa hatima yake iko mikononi mwa taifa la Marekani.
Tazama Video hapo chini( Video inatisha) .Video
hii imeanza na hotuba fupi ya Rais Obama . Baada ya hotuba
hiyo, Mwandishi huyo anawekwa mbele ya kamera na kuuawa kikatili.