POLISI mkoani Mwanza wamewatia mbaroni viongozi sita na wafuasi kadhaa wa CHADEMA
waliokuwa wakijiandaa kuandamana ikiwa ni hatua mara baada ya wanachama
hao kukaidi amri ya polisi iliyowekwa ya kusitisha maandamano.
Tukio
hilo limetokea leo majira ya saa 5.20 asubuhi muda mfupi baada ya
wafuasi hao kujipanga kuanza maandamano yaliyokuwa yaanzie Viwanja vya
Sahara mkoni Mwanza hadi Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana zilizopo
katikati ya na kufanya mkutano mfupi wa hadhara kufikisha ujumbe
uliokusudiwa.
Katika
purukushani hiyo iliyodumu zaidi ya masaa mawili huku ikiambatana na
wafuasi hao kupigwa virungu, Polisi wamewatia mbaroni watu takribani 14
wanaodaiwa kuandamana bila kibali.
Aidha Polisi
walionekana kutanda kwenye maeneo mbalimbali jijini hapa wakiwa na
silaha za moto na mabomu ya machozi huku gari la maji ya kuwasha nalo
likipita mitaa kadhaa ya barabara muhimu kuashiria kuwasaka
waandamanaji.
Licha ya
kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado
halijatoa taarifa kamili na idadi ya watu inayowashikilia.
 |
Polisi
wakipita katika mtaa wa Kemondo na Nyerere kufanya doria kufuatia
taarifa za maandamano ya CHADEMA kutangazwa jijini Mwanza. |
 |
Polisi katikati ya mji wa Mwanza wakifanya doria. |
 |
Ingawa
kuna ukimya lakini kuna taarifa za kichini chini zikisema, Inasemekana
waandamanaji watatumia style tofauti kukusanyika kwenye ofisi mbili
walizozitaja, moja wapo ikiwa ni Ofisi ya Mkuu wa Wilaya au Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa, wakitoka pande mbalimbali za mji. |
 |
Polisi wakiwashusha kituoni baadhi ya viongozi wa CHADEMA waliowakamata. |
 |
Hatua kwahatua. |
 |
Mpaka ndani. |
 |
Katibu wa Baraza la Wanawake Wilaya ya Ilemela CHADEMA akizungumza na waandishi wa habari amesema bado maandamano yataendelea na hayatokoma mpaka ujumbe |
0 Comments