NIWASHUKURU wote
tulioanza nao makala haya ambayo mwigizaji Wastara Juma amekuwa
akifunguka kuhusiana na maisha yake, bila shaka kwa namna moja au
nyingine tutakuwa tumejifunza kitu kupitia maisha yake.
Leo tunamalizia sehemu ya mwisho ya
makala haya, tutaona jinsi gani alikutana na aliyekuwa mumewe, marehemu
Juma Kilowoko ‘Sajuki’. Twende pamoja:
Mwandishi: Ulikutana lini na Sajuki na wapi?
Wastara: Nilikutana na Sajuki mwaka 2007
kwenye kazi ya filamu ambapo tulikuwa marafiki sana, mara nyingi
tulikuwa tunakaa na kuzungumza stori za maisha huku kila mmoja
akimweleza mambo aliyopitia katika mapenzi, ile filamu ilipoingia tu
sokoni tukaanzisha uhusiano kwani kila mtu alikuwa na ‘stress’ za
mapenzi na kila mmoja alikuwa ameshajua anachokipenda na anachokichukia
mwenzake.
Wastara: Kwa hiyo uhusiano tuliuanza rasmi mwaka 2008 ambapo tulikaa mpaka 2009
0 Comments