Mwanamke
nchini Ufaransa, juzi amefunga ndoa na mwanae wa kambo baada ya
kusuguana na mamlaka za nchini humo kuhusu haki yake ya kuolewa.
Elisabeth Lorentz, 48, amefunga ndoa na Eric Holder,
kanisani kwenye kijiji kidogo Dabo huko Alsace-Lorraine, kaskazini
mashariki mwa Ufaransa. Ms Lorentz alikutana na baba yake na Holder
mwaka 1989, wakati huo akiwa na miaka 24.
Wawili hao walipata mtoto wa kike mwaka 1997 – ambaye ni dada yake na Holder lakini pia mtoto wake wa ubatizo.
Holder
pia alikuwa na mtoto kipindi hicho. Ms Lorentz aliolewa na baba yake
Holder mwaka 2003, lakini walitengena baada ya miaka mitatu.
Ms
Lorentz ameviambia vyombo vya habari kuwa baada ya kuachana na mume
wake, mwanae wa kike ambaye alikuwa na miaka 9 aliumizwa vibaya na
alikuwa akilia kila siku. “Hapo ndipo Eric akawa msaada mkubwa kwetu na uhusiano ulizaliwa,” alisema.
Holder,
ambaye anasema alijitahidi kumliwaza dada yake aliyekuwa pia mtoto wake
wa kuzaliwa na sasa mwanae wa kambo, alisema: ‘Baada ya baba kumwacha mama, nilihisi kutengwa. Nilijua alivyojisikia.
Haikuchukua
muda Holder akaamua kumwomba uchumba mama yake wa kambo. Hata hivyo
walikumbana na kikwazo kwakuwa sheria za Ufaransa zinakataza ndoa ya
watoto na wazazi wa kambo.
0 Comments