MWALIMU wa Shule ya Sekondari ya Muungano iliyopo mji mdogo wa Himo wilayani Moshi, Richard Ndoile (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, kwa tuhuma za kukutwa gesti na mwanafunzi wake wakifanya mapenzi.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita alisema jana ofisini
kwake, kuwa tukio la kukamatwa kwa mwalimu huyo lilitokea Oktoba 4, saa
5.00 asubuhi, katika gesti ya Kilimanjaro iliyopo Himo.
Moita
alisema mwalimu na mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) ambaye anasoma
Shule ya Sekondari Muungano Kidato cha Tatu, walikamatwa baada ya wazazi
wa mwanafunzi kumuona binti yao akiwa amepakiwa kwenye pikipiki ya
mwalimu wake, kuelekea mahala kusikojulikana.
Alisema hatua hiyo iliwafanya kuhamaki na hivyo kuanza kufuatilia mwelekeo wa pikipiki ili kujua hatma ya safari yao hiyo.
Alisema
baada ya kuwafuatilia, pikipiki hiyo ilielekea kwenye gesti hiyo na
baada ya kuteremka mtuhumiwa na binti yao waliingia ndani na kuchukuwa
chumba, kwa lengo la kutimiza haja zao.
Kwa
mujibu wa Kamanda Moita, wazazi waliamua kupiga simu katika Kituo
Kidogo cha Polisi cha Himo kwa lengo la kutoa taarifa, ambapo polisi
walifika lakini hadi mtuhumiwa anakamatwa tayari walikuwa
wameshatekeleza tendo la kujamiiana.
Alisema
mwalimu huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha
Himo, kwa ajili ya kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili
0 Comments