Mwanamume
ambaye kazi yake ni ya upishi nchini Australia, anadaiwa kumuua mpenzi
wake na kumkatakata vipande na kupika baadhi ya sehemu zake za mwili.
Aliyafanya unyama huo kabla ya yeye mwenyewe kujitoa uhai wake.
Marcus
Volke, mwenye umri wa miaka 28, alijikataa koo yake huku akiwatoroka
polisi waliokuwa wamekuja kufanya uchunguzi baada ya majirani zake
kuripoti kuwepo harufu mbaya mfano wa nyama iliyooza iliyokuwa inatoka
nyumbani kwa mwanamume huyo.
Maafisa wa polisi walipata sehemu za
mwili wa mwanamke huyo zikitokota kwenye sufuria iliyokuwa imejazwa
kemikali huku vipande vingine vikiwa kwenye karatasi za plastiki za
takataka nje ya nyumba katika mtaa wa kifahari za Teneriffe.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Brisbane Courier Mail. Mwanamke huyo raia wa Indonesia bado hatajambulishwa rasmi.
Wapenzi hao waliokuwa wanaishi pamoja walikutana wakiwa wanafanya kazi kwa meli za kifahari na wote walikuwa wameajiriwa.
Wakazi
wa mtaa huo waliambia vyombo vya habari kuwa harufu mbaya ilikuwa
inatoka katika myumba ya Volke na ikazidi kuwa mbaya siku ziliposonga.
"nilipotoka
nje harufu hiyo ilisababisha machozi kutoka machoni na hata kunifanya
kujihisi mgonjwa,'' alisema mkazi mmoja. ''Ungedhani chakula cha Mbwa au
nyama ilikuwa imeachwa nje kwa siku kadhaa.''
Polisi wangali wanafanya uchunguzi.
0 Comments