Wajukuu wa marehemu Sabina Ngalu wa Mwanza wamecharazwa viboko na
watoto wa marehemu baada ya kung’ang’ania kaburini wakitaka wapewe
fedha.
Chanzo cha wajukuu hao zaidi ya 10 kucharazwa bakora ni kung’ang’ania
ndani ya kaburi lililokua limeandaliwa kwa ajili ya kuhifadhi mwili wa
marehemu wakitaka wapewe ng’ombe mmoja au sh.100,000 kama zinavyotaka
mila za kabila la kisukuma.
Gazeti la MTANZANIA ambalo lilikua shuhuda katika eneo hilo lilisema
kitendo hicho kilimkera Padri Nicodemus Mayalla aliyekua eneo hilo huku
akiwataarifu polisi kuhusu vurugu hizo hata hivyo kaka mkubwa wa
marehemu aliamua kuchukua fimbo na kuanza kuwachapa.
Kitendo cha kuwachapa kiliamsha hasira zaidi kwa wajukuu hao ambao
nao walijibu kwa kurusha michanga wakiwa ndani ya kaburi hadi
waombolezaji walipoamua kuchanga na kuwapa fedha hizo ndipo walipotoka.
0 Comments