![.](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vdH3DbEM_ieUi13Xi_hJVNikoK3GAjlCicmvxJ7Juok2WIrZ6bZzWYb0BG6lzSNZe_bYa2F5A7XzZPq_SOdpph2EM7aVy2PCzifLHedzVTbMYApqcZ2Z41dhxbQVtghv8o6iSKTSiyXjor_eXtXjKvIKYbP-52ucQfVQ=s0-d)
.
Miongoni mwa story zilizochukua headline Jan 2 ni kuhusu kikundi cha watu maarufu kama
‘Panya Road’ kilichovamia maeneo mbalimbali, kupora vitu vya thamani na kupiga watu.
Staa wa kike wa
Bongo Fleva Rehema Chalamila aka
Ray C kupitia instagram amethibitisha kuwepo kwa kikundi hicho cha uhalifu na kuandika ‘
Sina
hamu na hawa panya road, jana nilikuwa sehemu flani sinza nakula
kitimoto nilivyoona watu wanakimbia nikatoka nduki bila viatu nikaingia
kwenye gari mbio mara mbele yangu nikakutana na lundo la watu wakinoa
mapanga barabarani, niligeuza gari utafikiri niko kwenye movie
nikajikuta nimefika osterbay polisi bila viatu mpaka askari wakanicheka!
!!!!!!!!!!Serikali tunaomba mkamate hawa vijana kwakweli maana tumezoea
amani sasa mambo kama haya yakitokea yanakosesha amani kabisa kwa
wananchi!Na uhakika Jeshi la polisi litafanya kazi yake yani nilijihisi
kama niko Rwanda maana nakumbuka mapanga yale niliwahi yaona kwenye muvi
ya Somewhere in April na Hotel Rwanda!!!!Sasa wale waliosema bora damu
imwagike nadhani kauli itabadilika maana kama Panya Road wanatupelekesha
hivi je hiyo Vita!!!, Je hiyo vita, si tutapanda juu ya nyumba
zetu!!!!! Jamani msicheze na haya mambo jamani, amani ndio sifa kuu ya
nchi yetu……..Eeh Mungu tuepushe na haya mambo……’aliandika
0 Comments