Klabu ya jijini London ya Arsenal itatangaza kumsajili kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira baada ya kufikia makubaliano na wawakilishi wa mchezaji huyo pamoja na viongozi wa Real Madrid.
Khedira kwa muda mrefu amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Real Madrid hasa baada ya kusajiliwa kwa kiungo Toni Kroos na klabu ya Arsenal imekuwa ikisaka saini ya kiungo huyu ili kuboresha idara yake ya kiungo.
Kwa mujibu wa taarifa toka Hispania na England, Arsenal
imekubali kulipa paundi milioni 11 kwa ajili ya kiungo huyu mwenye
asili ya Tunisia ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha cha Ujerumani
kilichotwaa ubingwa wa dunia nchini Brazil mwaka jana.
Khedira angeweza kuondoka tangu wakati wa usajili wa majira ya joto lakini Arsenal na Madrid
zilishindwa kufikia makubaliano juu yake na moja kati ya nafasi ambazo
zimekuwa zikimtatiza kocha Mfaransa ni nafasi ya kiungo ambayo Khedira endapo akiwa fiti atakuwa na uwezo wa kuiboresha.
0 Comments