Star wa Ivory Coast anayechezea klabu ya Chelsea, Didier Drogba
anatarajiwa kutangaza kustaafu kuichezea klabu hiyo mara baada ya
kumalizika kwa msimu huu akiwa amerejea Chelsea akitokea Galatasaray ya
Uturuki.
Drogba ambaye kwa Chelsea anahesabika kama gwiji au ‘Legend’ ametengenezewa nafasi ya kubaki ndani ya klabu hiyo mara atakapostaafu ambapo ataendelea kuwepo chini ya kocha Mreno, Jose Mourinho.
Drogba anatarajiwa kukaa kwenye benchi la Chelsea akiwa mmoja wa makocha wasaidizi wa Mourinho jukumu ambalo nyota huyu wa Afrika amekubali kulichukua baada ya kukubali kuwa hawezi kuendelea kucheza katika kiwango cha juu.
Drogba alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Olympique Marseille
mwaka 2003 ambapo aliichezea klabu hiyo kwa miaka 9 ambapo alifanikiwa
kutwaa mataji kadhaa huku akijijengea sifa ya kuwa nyota wa mechi kubwa
kutokana na uwezo wake w akufunga mabao muhimu kwenye mechi kubwa
zikiwepo hatua za nusu fainali na fainali.
Drogba alirudi Chelsea msimu huu baada ya kuondoka mwaka 2012 wakati klabu hiyo ilipotwaa ubingwa wa ulaya baada ya kuifunga Bayern Munich ya Ujerumani huku Drogba akifunga penati ya mwisho iliyoipa Chelsea ubingwa.
0 Comments