Klabu ya Arsenal imemruhusu mshambuliaji wake Lukas Podolski kujiunga
na mabingwa wa zamani wa ulaya Inter Milan zikiwa zimepita siku chache
tangu kocha wa Arsenal Arsene Wenger akanushe taarifa za mshambuliaji
huyo kuondoka.
Podolski anajiunga na Inter baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye
kikosi cha kwanza cha Arsenal ambapo mara nyingi amejikuta akiwa
mshambuliaji wa akiba ambaye mara zote amekuwa akitokea benchi pamoja na
kuwa na rekodi nzuri ya kufunga kulingana na nafasi ndogo anayopewa.
Lukas Podolski ameondoka Arsenal na kujiunga na Inter Milan baada ya kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.
Mshambuliaji huyo Mjerumani ataichezea Inter kwa mkopo wa miezi sita
na baada ya hapo atakaa chini na uongozi wa klabu hiyo na kuchagua kama
angependa kujiunga nao moja kwa moja.
Siku chache zilizopita kocha wa Arsenal Arsene Wenger alikanusha
taarifa za kuondoka kwa Podolski baada ya kuulizwa na waandishi wa
habari ambapo jibu la kocha huyo mfaransa lilikuwa ‘hapana Podolski
hataondoka’.
Lukas Podolski akiwa na mashabiki wa Inter Milan kwenye uwanja wa ndege wa Milan baada ya kuingia akitokea London juzi.
0 Comments