Mtoto aliyefanyiwa ukatili na baba yake |
Mkazi mmoja aishiye katika Kitongoji cha Buyumba,Kijiji cha
Bushemba,Kata ya Buganguzi Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera aitwaye Godfrey Joseph Kajuna (45miaka) amejinyonga hadi kufa
baada ya kumfanyia ukatili mtoto wake wa kumzaa.
Inasemekana
kuwa baba huyo alimpiga na kumjeruhi kichwani
kwa fimbo nzito kisha akamtoboa macho, mtoto huyo aitwaye Agripina
Godfrey (12) anayesoma darasa la Kwanza katika shule ya msingi Ilambika.
Chanzo cha habari hizi kinasema kisa kizima ni kwamba Baba alitoka ndani na kuwaambia wanae kuwa Mama yao akirudi wasimfungulie mlango…
Chanzo cha habari hizi kinasema kisa kizima ni kwamba Baba alitoka ndani na kuwaambia wanae kuwa Mama yao akirudi wasimfungulie mlango…
Hivyo mama aliporudi watoto kwa kumuogopa Baba yao wakakataa kata kata kumfungulia Mlango.
Basi Mama akaondoka kujiweka sehemu.
Baba yao aliporudi akawauliza Mama yao yuko wapi,ndipo huyo mtoto aliyeonekana kama ndiyo mkubwa kwenye familia hiyo akamjibu Baba yake kuwa "Baba si ulisema mama akija tusimfungulie?" Hali hiyo ikamfanya Baba yake aanze kumpiga sana! Mpaka kumuumiza vile.
Sasa damu zikaanza kumtoka mtoto,Baba mtoto akachukua Chumvi na kuanza kuimimina kwenye jeraha kichwani
Basi mtoto alipoonekana kama hali inakuwa Mbaya… Baba akaandika kijibarua haraka na kusema kuwa kwa kitendo alichofanya na vitendo vingine ambavyo huwa anaifanyia familia hiyo ameogopa kukamatwa… akajitundika kwenye Kamba na kujimaliza yeye mwenyewe. Mtoto alipelekwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Muleba (Rubya Hospital) kwa matibabu zaidi.
0 Comments