Mwanaume
mmoja Nigeria amefunguliwa mashtaka baada ya kumfungia mke wake nje ya
nyumba yao mpaka asubuhi na kuamua kumbaka mtoto wake wa kike mwenye
umri wa miaka 9.
Polisi wamemfungulia mashtaka mwanaume huyo ambaye jina lake ni Osaro mwenye umri wa miaka 55 baada ya kuripotiwa kufanya kosa hilo.
Mama wa mtoto huyo Stella,
aliwaambia wachunguzi wa tukio hilo kuwa mumewe alimfungia nje ya
nyumba yao saa 2 usiku na yeye kujifungia ndani na mabinti zake wawili.
Siku iliyofuata mtoto huyo alimwambia
mama yake kuwa alifanyiwa kitendo hicho na baba yake zaidi ya mara moja,
mama huyo akamkagua na kubaini ni kweli alibakwa.
0 Comments