Staa
wa urembo, muziki, filamu na ujasiriamali Bongo, Jokate Mwegelo
‘Kidoti’ au ‘Jojo’ amemrushia maneno makali aliyewahi kuwa mpenzi wake,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa hana akili timamu kufuatia maneno
aliyotoa kuwa enzi za uhusiano wao, eti mwanadada huyo alikuwa akichenga
kumzalia mtoto.
Katika
mahojiano maalum ya hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mtu Kati cha
Runinga ya GlobalTV Online, Diamond alitoa madai kuwa, amekuwa akihaha
kupata mtoto.
Alisema
kwamba, katika harakati zake hizo, warembo ambao alishatoka nao
kimapenzi akiwemo Jokate walikuwa wakimchezea mchezo mchafu ili
wasimzalie kwa kuwa alikuwa akiwaambia anahitaji mtoto kwa udi na
uvumba.
Hata
hivyo, madai hayo ya Diamond yalizua mzozo mkubwa kwenye mitandao ya
kijamii huku warembo hao wakipigwa za uso hivyo kutafuta namna ya
kujitetea.“Hao akina…(wanatajwa warembo wa Diamond) watakuwa wana
matatizo ya uzazi siyo bure.
“Ndiyo
maana Dangote (Diamond) ameona bora aende kwa Zari (msanii wa Uganda,
Zarinah Hassan) ambaye tayari ana mwanga wa kuzaa (ana watoto watatu),” ilisomeka sehemu ya maoni juu ya madai hayo ya Diamond kwenye Mtandao wa Instagram.
Diamond alifunguka:
“Jokate na Wema (Sepetu) nilitamani sana wanizalie lakini walikuwa
wakichengachenga, mambo mengine ujue si ya kuzungumza lakini inauma.”
Kufuatia
tuhuma hizo nzito huku kukiwa na madai pia, kwamba Jokate aliwahi
kupigwa mimba ‘akaipanchi’, mwanadada huyo alipotafutwa na mwandishi
wetu kujibu ‘shitaka’ linalomkabili alianza kwa kumshangaa staa huyo wa
Ngoma ya Ntampata Wapi inayokimbiza kwa sasa.
Jokate
alisema anamshangaa Diamond kuyazungumza maneno hayo hadharani na
inaonesha asivyokuwa na akili timamu au ambayo haijakomaa.
“Diamond atuache, kila siku anatuzungumzia, hana akili timamu.
“Inadhihirisha
kweli hana akili kwa kuwa mtu mwenye akili zake timamu hawezi kwenda
kwenye chombo cha habari na kueleza hayo aliyoyasema,” alisema Jokate akionesha kukasirishwa na maneno ya Diamond.
Ukiacha
Jokate na Wema ambaye naye aliwekwa kwenye kapu moja la kuchenga
kumzalia, hakutaka kumjibu Diamond kwa kuwa hataki malumbano au makuu na
mtu.
Pia
jamaa huyo alimzungumzia aliyekuwa mwandani wake mwingine, Penniel
Mwingilwa ‘Penny’ kuwa yeye alitoa mimba zake mbili kwa visingio
tofauti.
Katika majibu yake, Penny alisema kuwa Diamond awe mkweli na aseme tatizo lake kwani anavyojua yeye hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.
Katika majibu yake, Penny alisema kuwa Diamond awe mkweli na aseme tatizo lake kwani anavyojua yeye hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.
0 Comments