Stori
ambayo imechukua nafasi kubwa ya kujadiliwa kuanzia mida ya jioni Dar
es salaam ni kuhusu kikundi cha wezi wanaotumia ubabe maarufu kama Panya
Road ambacho kinaaminika kuvamia maeneo kadhaa ya Dar es Salaam ikiwemo
Sinza, Mwananyamala, Tabata na sehemu nyingine.
Taarifa ambazo zilianza kusambaa kutoka kwa mashuhuda ni kwamba Wezi
hawa walikua wakipiga watu, kupora vitu mbalimbali na hata kuharibu
baadhi ya magari na pikipiki kwa kuvunja taa wakati wakipita kwenye
mitaa mbalimbali.
Baada ya taarifa kusambaa Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es
salaam Suleiman Kova alizungumza kwenye TBC1 na kusema hawezi kupinga
uhalifu kufanyika leo mtaani lakini sio kwa kiasi hicho ambavyo
imeripotiwa, yaani habari imekuzwa kuliko ukweli wenyewe.
Miongoni mwa waliothibitisha tukio la magari kuvunjwa taa na wenye
magari kuyaacha kandokando ya barabara magari hayo ni producer wa
bongofleva Sheddy Clever alietengeneza hits kama ‘number one‘ ya Diamond Platnumz.
Mwingine aliekumbwa na huu mkasa ni mtangazaji wa Clouds FM Efphraim
Kibonde kama ambavyo wote wanasikika wakizungumza kwenye hizi sauti hapa
chini.
0 Comments