.
Baada ya msanii wa Hip Hop
Nikki Mbishi aka Baba Malcom kutangaza kuwa ameacha kufanya kazi ya
muziki sasa Chid
Benz amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa ameshafanya mazungumzo na
msanii huyo na kumtaka asichukue uamuzi huo mapema kwani hata yeye
amepitia katika changamoto hizo.
Chid Benz alichukua nafasi hiyo kuwataarifu mashabiki wa muziki kupitia ukurasa wa
facebook na kuandika ‘Nakanusha
habari za Nikki mbishi kuacha mziki,nimeongea nae kama kaka na kumgusia
mengi,najua amenielewa na nimemwambia asikubali wale wanaomkubali
waanze kukubali wengine.mimi nimekumbana na vingi na watu weengi
waliaminishwa kama nimeshushwa kimziki,jimefanyiwa mengi ambayo kwa muda
ule nsingeweza kuelezea kila mtu nini kinaendelea,so if kikitokea
kibaya kinatangazwa mpk kwenye taarifa za habari mbona mziki
hauchezwi?ningekua sina nguvu hio nisingesumbua watu kuniweka front
page..but bado nipo na nimekomaa.na naishi na naona wanaopewa kipaumbele
na najua bado mimi ni mimi.Iron
.
0 Comments