Advertisement

Responsive Advertisement

Kamanda Kova amezungumza kuhusu malalamiko ya picha za wasiohusika kuonyeshwa kama wahalifu wa #PanyaRoad


aff6SAM_3898 kovaaaaaaaaaaaaa
Moja ya story ambazo zimechukua headlines siku ya leo ni ishu ya watu kadhaa kulalamikia kwamba picha zao zimeonekana kwamba wao ni watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa kujihusisha na kundi la Panya Road.
Leo katika kipindi cha XXL ya Clouds FM, Kamanda wa Polisi Suleiman  Kova ameongelea story hiyo; Kuna mtu aliniuliza swali siku ya leo, mimi mwenyewe nilitoa picha tatu kwamba hao ndio realy leaders ile ya Press Conference tuliyofanya, baada ya hapo sijatoa tena picha nyingine, isipokuwa ninachofahamu mimi ni kwamba badae nikaona kwenye gazeti hilo kuna picha yangu mimi ambayo sikupigwa siku hiyo au jana yake nikaona kuna picha nyingine, zote ni za zamani hizo.
Sasa inawezekana mle ndani huyo kijana yumo lakini jibu ni kwamba hiyo ni kazi ya waandishi wa habari… yani ninyi huwa mna taratibu zenu kwamba likitokea tukio fulani labda liwe la michezo au la vita mnachukua background picha ambazo zipo unaona sasa mimi tena siwezi kulaumiwa kwamba eti hizo picha zinanihusu mimi, mbona hata mimi ya kwangu ilitoka nikiwa na cheo cha Senior Assistant Commissioner… lakini nimekubali tu kwa sababu najua cha muhimu pale ni message kwa wananchi kwamba kuna suala la panya road na hata kuna wengine walishakamatwa siku za nyuma.
Kwa hiyo sisi Polisi hatuwezi kuendelea kulaumiwa kwamba kwa nini hizo picha zimeonekana… sie hatujazipeleka, tulizozipeleka ni tatu tu ambazo hao watu hawajalalamika, kwa hiyo kama wakitaka huyo bwana aulizwe kwanini wamemchapisha kwanza nyinyi sasa ndio mnatakiwa muwaeleweshe hawa raia kwamba hizo picha ni kawaida yetu sisi huwa tunazitoa hivyo ilimradi ni ishu ambazo zina mahusiano, unakuta mmetoa picha za Rais za miaka mitatu iliyopita au Waziri… au mtu yoyote yule unatoa kwani ukitoa zile atasema mbona sijapigwa picha?“– Suleiman Kova.

Post a Comment

0 Comments