Jana kulikuwa na sherehe kubwa Afrika,
Ulimwengu wa soka ulikuwa macho kufuatilia tukio zima la utoaji wa Tuzo
ya Mchezaji Bora Afrika ambapo Shirikisho la Soka Afrika, CAF ndio
walikuwa waandaaji na watoaji wa Tuzo hizo, Yaya Toure aliibuka kuwa mshindi wa Tuzo hiyo.
Msanii Diamond Platnumz alipata nafasi kuwa mmoja ya wasanii walioperform kwenye sherehe hizo, pamoja na P Square.
Kuna picha zikionyesha Diamond akipiga acapella na washkaji wa P Square na Flavour walipokutana Nigeria.
0 Comments