Wafanyabiashara
Abubakar Kasanga (28) na Ezekiel Kaseregela (25), wamefikishwa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi mbili tofauti za mauaji ya
kukusudia ya wanawake waliokuwa wakifanya nao mapenzi.
Inadaiwa
kuwa Kasanga na Kaseregela walikuwa wakiwarubuni wanawake kadhaa,
kufanya nao mapenzi na kutumia mwanya huo kuwalewesha dawa, kuwaibia na
kuwaua.
Akiwasomea
shtaka la mauaji katika kesi PI namba 1, Wakili wa Serikali, Janeth
Kitali alidai kuwa Novemba 14, 2014, Kasanga aliyekuwa akiishi nyumba ya
wageni na Kaseregela akiishi Tandika, walimuua kwa makusudi Jacqueline
Masanja.
Baada
ya kusomewa shtaka hilo linalowakabili, Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda
aliwaeleza washtakiwa hao kuwa hawaruhusiwi kuongea chochote mahakamani
hapo kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kulisikiliza shtaka hilo
isipokuwa Mahakama Kuu.
Na Tausi Ally, Mwananchi
0 Comments