Mkali wa Movie za matukio ya mapigano au Action Movies, Sylvester Stallone ametangaza ujio wa filamu yake mpya itakayokuwa sehemu ya mwisho ya mfululizo wa filamu za Rambo ambazo zimemjengea umaarufu kiasi cha watu kumpachika jina la Rambo.
Stallone alithibitisha habari hizi kutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter ambapo alikuwa akizungumza na mashabiki wake ambao aliwaambia kuwa sehemu ya mwisho ya filamu za Rambo itaanza kutengenezwa mwaka huu.
Filamu hii ambayo itapewa jina la Rambo The Last Blood inamuonyesha mkongwe wa vita ya Vietnam, John Rambo
akiwa kwenye harakati zake za mapambano na filamu hii haitakwenda mbali
na story ya filamu hizi ambazo sehemu yake ya kwanza iliigizwa mwaka
1982 katika filamu iliyoitwa Rambo First Blood.
Mwaka 2015 unatarajiwa kuwa mwaka ambao Stallone
atakuwa ‘Busy’ akitengeneza filamu tatu tofauti ikiwemo Scarpa ambayo
ataanza kuitengeneza mara tu baada ya Rambo Last Blood kumalizika na pia
anatarajia kutengeneza sehemu nyingine ya filamu za Rocky Balboa ambapo safari hii ataigiza kama kocha wa mjukuu wa mpinzani wake wa zamani ulingoni Apolo Creed.
Rambo
ambaye ana umri wa miaka 68 amesema kuwa amelazimika kufanya mazoezi
makali ili kutengeneza mwili wake kuendana na uhusika wa sehemu
atakazokuwa akiigiza ili aweze kuendana na story halisi zilizomo kwenye
filamu hizi hasa ukizingatia kuwa filamu anazotengeneza ni za mapigano
na utimamu wa mwili na matumizi ya nguvu nyingi ni jambo la lazima.
0 Comments