Taarifa kutoka Kenya zinasema mashuhuda wengine wanne wa kesi ya inayomkabili Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto katika Mahakama ya ICC wamepotea katika kaunti ya Uasin Gishu, Kenya.
Hili limetokea siku chache baada ya shahidi mwingine Meshack Yebei
kuuawa katika mazingira ya kutatanisha, huku ndugu wakisisitiza kutaka
kufanya mazishi ya mtu huyo kinyume na uamuzi wa Mawakili wa William Ruto ambao wanataka mwili huo ufanyiwe uchunguzi kwa kuwa marehemu alikuwa mmoja ya mashahidi muhimu wa kesi hiyo.
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Kenya, Ken Wafula amewataja mashuhuda wa kesi ya Ruto waliopotea ni Yohana Kimng’etich Bureti, Benjamin Kipchumba, Phillip Arusei na mwingine aliyetambulika kwa jina moja la Miriam.
Watu mbalimbali pamoja na Wabunge wa Jubilee wamemtaka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Kenya kumchunguza Wafula wakimtuhumu kuhusika na tukio la mauaji ya Yebei, huku Wafula naye akiishitumu Serikali kuhusika na matukio ya mauaji na upoteaji wa watu hao.
0 Comments