HATIMAYE ukweli
wa kutekwa, kuteswa kwa kudhalilishwa kwa aliyekuwa mume wa mwimba
taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan
‘Tevez’, umejulikana.
Mfanyabiashara, Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa amefungwa kamba na watesi wake.
Januari 28, mwaka huu, picha za Tevez akiwa ametoka kuteswa kwa
kudhalilishwa zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku
wengine wakidai kisa ni kukutwa na mke wa mtu, wengine wakisema ni
dhuluma.
RISASI LAINGIA MTAANI KUCHIMBA
Risasi
Jumamosi halikufanya haraka kuichapisha habari hiyo mpaka kuichimba
kwanza ili kujua kisa na mkasa kamili ndipo iwapelekee wasomaji wake. Na
ndivyo ilivyofanyika!
ENEO LA TUKIO
Risasi
Jumamosi lilichimba na kubaini kuwa, tukio la Tevez kufanyiwa ukatili
huo lilitokea kwenye mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambako alikwenda
kibiashara.
“Tukio
si la Dar kama wanavyosema wengine, limetokea mjini Durban, Afrika
Kusini. Si unajua jamaa (Tevez) ni mtu wa tripu za kibiashara!” alisema
mtoa habari mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.
Jeraha likiwa mgongoni mwa Jumanne Hassan ‘Tevez’ baada ya kuteswa.
WALIOFANYA UKATILI
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, watu waliomtenda Tevez ni jamaa zake anaofanya
nao biashara ambayo Risasi Jumamosi halijaijua vizuri (ingawa kwenye
mitandao ya kijamii wanadai ni madawa ya kulevya).
YATAJWA DHULUMA
Chanzo kikaanza kuanika historia nzima tangu Tevez hajafanyiwa utekaji na udhalilishwaji huo.
“Siku
za nyuma Tevez alipewa mzigo nchini Tanzania ili awapelekee hao jamaa
wa Afrika Kusini. Aliondoka jijini Dar kwenda Nairobi, Kenya kwa basi
akiwa na begi.
“Alipofika
Nairobi, ilidaiwa begi hilo alilisahau kwenye basi lakini wengine
wanasema aliuuza Nairobi na kwenda Afrika Kusini akiwa na begi feki.”
TEVEZ AWASILI AFRIKA KUSINI, AKUMBANA NA MSALA
Habari
zaidi zikachimbuka na kudai kwamba, Tevez aliwasili mjini Durban na
kukutana na jamaa zake ambapo aliwaambia mzigo aliusahau kwenye basi.
“Kumbe
inasemekana jamaa aliyemuuzia mzigo Nairobi anafahamiana na jamaa wa
Sauz na aliwapigia simu kuwaambia kwamba, ameuziwa mzigo na Tevez.
“Kwa hiyo mpaka Tevez anawasili kule, jamaa walikuwa wanajua hana mzigo kwa kuwa aliuuza Nairobi,” kilisema chanzo.
‘Tevez’ akiwa na moja ya wadau wenzake katika biashara anazofanya huko Durban.
ATEKWA, ADHALILISHWA
Ikaendelea
kudaiwa kuwa, madai ya Tevez yaliwakera jamaa kwa vile walijua kila
kitu, hivyo walimteka na kuanza kumtesa kwa kumvua nguo zote, wakamfunga
kamba za manila za rangi ya bluu na kuanza kumtesa kwa adhabu
mbalimbali ili kumkomesha.
Inadaiwa
katika adhabu hiyo, jamaa hao walimpiga na kitu chenye ncha kali hali
iliyosababisha Tevez atokwe na damu na ngozi kuchubuka eneo la mgongoni.
MADAI WAKATI WA UDHALILISHWAJI
Inadaiwa wakati udhalilishaji huo ukiendelea, jamaa hao walikuwa wakisema wanachotaka ni mzigo wao na si kitu kingine.
MARAFIKI, JAMAA WA DAR
Kufuatia
kusambaa kwa picha hizo mtandaoni, marafiki na jamaa wa Tevez waliopo
Bongo walilazimika kufanya mpango kwa kuwasiliana na watu wa karibu
waliopo Durban kumnusuru Tevez kwa kumpeleka hospitali ambako anapata
matibabu hadi juzi, Alhamisi.
Risasi Jumamosi: “Kuna habari alikatwa sehemu za siri ni kweli?”
Chanzo: “Si kweli.”
Risasi Jumamosi: “Inasemekana alifanyiwa kitu mbaya cha mambo ya Sodama, ni kweli?”
“Si kweli. Watu wanasema tu. Ila walimtesa sana kwa kweli.”
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa na moja ya jamaa zake sauzi.
RISASI LATINGA DUKANI KWA MKEWE WA SASA
Ili
kuzidi kupata habari zaidi, Januari 28, mwaka huu, usiku Risasi
Jumamosi lilikwenda Kinondoni Kwamanyanya, Dar kwenye duka la mke wa
sasa wa Tevez ili kumsikia anasema nini kuhusu tukio hilo.
Paparazi wetu hakumkuta mke huyo lakini alibahatika kuongea na msichana aliyekuwa nje ya duka hilo na kumuuliza aliko Tevez.
Msichana: “Tevez yupo safarini Morogoro.”
Risasi Jumamosi: “Mbona hapatikani hewani? Nipe namba zake nyingine.”
Msichana: “Nilizonazo ndiyo hizohizo ulizonazo wewe, ni…(akazitaja).”
Kweli namba hizo ndiyo alizokuwa nazo paparazi wetu.
MAMA MKWE WA TEVEZ
Kesho
yake, Risasi Jumamosi lilimsaka kwa simu mama mkwe wa zamani wa Tevez
(mama wa Isha) lengo ni lilelile, kutaka kujua kama naye ana taarifa
hizo na anasemaje.
“Ni
kweli nimesikia na nimeona picha zake yaani nimesikitika sana kiasi
kwamba nikawa siamini kama ni kweli yeye anaweza kufanyiwa ukatili wa
aina hiyo.
“Kikubwa
namshukuru Mungu kusikia yupo hai na kwa maana hiyo namuombea zaidi ili
arudi katika afya yake,” alisema mama mkwe huyo aitwaye Rukia Juma.
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’akiwa na mkewe.
MTU WA KARIBU NA TEVEZ
Risasi
Jumamosi liliendelea kutafuta undani zaidi wa tukio la Tevez kwa
kuongea na watu wake wa karibu waliopo Durban, ndipo likapenyezewa ishu
mpya kuwa, baadhi ya ndugu na wafanyabiashara wenzake na Tevez
wamechanga na kurudisha mali zilizokuwa zikidaiwa na jamaa hao.
“Nilikuwa
Durban muda si mrefu na hapa ndiyo narejea nyumbani (Bongo). Kiukweli
tukio la Tevez ndiyo habari ya mjini Sauz, maana jamaa wamemfanyia mbaya
kinoma lakini kusema kweli hajakatwa nyeti kama mitandao ya kijamii
inavyoandika, wamempiga sana.”
“Kingine ambacho ninajua tayari ameshatolewa kwenye jengo alilokuwa
ametekewa na sasa yupo hospitali maalum ambayo siwezi kukutajia, ila
huenda hali yake ikawa nzuri kama kweli atakuwa chini ya uangalizi wa
madaktari,” alisema jamaa huyo.
0 Comments