ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Zari.
ICON wa
Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati aliamua kumtolea uvivu,
aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’,
King lawrenc kwa kumuita mpuuzi anayetafuta kiki kwa vile kila kukicha
kazi yake ni kumfuatafuata kwa maneno ya kejeli na kumtusi.
X wa Zari, King lawrence akipozi.
Akipiga
stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, staa huyo alisema mara
nyingi amejitahidi kumpuuza kwa kitendo chake cha kumkejeli katika
mitandao ya kijamii, lakini kitu alichogundua ni kwamba mpenzi huyo wa
zamani wa Zari anataka yeye amjibu ili aweze kulikuza jina lake, kitu
ambacho ni cha kijinga.
Zarinah Hassani ‘Zari’.
“Nimejitahidi sana kukaa kimya kila anaponitusi huyu jamaa, lakini
kumbuka mimi ni binadamu, najaribu kuliangalia jambo hili nagundua
kwamba hana chochote cha msingi anachoongea zaidi ya matusi, anatafuta
nimjibu kitu ili apate kiki aweze kutimiza ndoto zake,” alisema Diamond
na kuongeza:
“Nashukuru nimegundua hana mada ya kuzungumza katika mitandao zaidi ya
mimi na Zari, ningemshauri aendelee na shughuli zake za kila siku,
asihangaike na kitu asichokijua, kugombana na mimi ni sawa na kumpigia
mbuzi gitaa, mimi nawaza nifanyeje ili niweze kuitangaza nchi yangu,
yeye anawaza afanyeje ili aweze kupandisha jina lake, siwezi kubishana
na mpuuzi.”
Mwanaume huyo Mganda, kwa muda mwingi amekuwa akiweka picha zake, Zari
na Diamond akisindikiza na maneno ya kejeli na dhihaka dhidi ya mkali
huyo wa Bongo Fleva, katika kile kinachoonekana kuwa ni kushikwa na
wivu.
0 Comments