Wakazi WA jiji la Dar es Salaam wako
katika hatari ya kupatwa na magonjwa makubwa kama saratani, utasa,
kupoteza uwezo wa kuona, kuharibu ubongo, maini na figo, kutokana na
matumizi ya mboga za majani zinazolimwa katika mabonde ya jiji hilo,
NIPASHE imebani
Matumizi ya mboga hizo ni makubwa jijini
humo, yakitokana na umuhimu wake kwa afya za watu na hali duni ya
maisha inayozifanya familia nyingi kumudu gharama zake ikilinganishwa na
vitoweo vingine.
Sehemu kubwa ya mboga hizo inatokana na
kilimo kinachofanyika kwenye bonde la Mto Msimbazi na maeneo ya
Kigogo-Sambusa, Ubungo–Gereji, Mchicha – Vingunguti na Tandale.
Tayari matokeo ya tafiti kadhaa
yamedhihirisha maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mboga za majani
jijini humo kuwa na kemikali zenye sumu ama taka zinazotoka viwandani na
kwenye makazi ya watu.
Pia, baadhi ya wakazi wanaoishi
pembezoni mwa bonde la Msimbazi na maeneo mengine yanayolimwa mboga
hizo, wamebainika kutupa taka kama betri zilizoisha muda wa matumizi,
masalia ya simu za mkononi, vipuri vya magari na majokofu mabovu.
Taka hizo zenye sumu kali, zinatupwa
kwenye mifereji ya maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mboga hivyo
kuzidi kuhatarisha afya za walaji.
TAFITI MBALIMBALI
Chuo Kikuu cha Ardhi (Aru), kilifanya utafiti katika bonde la Mto Msimbazi wilayani Ilala mwaka 2010, kwa kupima maji, udongo na maji, kwa vigezo vya Shirika la Afya Duniani (Who) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Chuo Kikuu cha Ardhi (Aru), kilifanya utafiti katika bonde la Mto Msimbazi wilayani Ilala mwaka 2010, kwa kupima maji, udongo na maji, kwa vigezo vya Shirika la Afya Duniani (Who) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Akizungumzia utafiti huo, Mhadhiri wa
Uhandisi wa Mazingira kutoka Aru, Dk. William Mwegoha, anasema
waligundua mabwawa ya majitaka yanayotoka Mabibo, dampo la Vingunguti,
viwandani na gereji mbalimbali yanamwaga maji kwenye mto huo.
“Baada ya kupima maji hayo, tulikuta yana madini ya shaba, risasi, kromiamu na ladimiamu ambazo ni sumu kwa mlaji,” anasema.
Dk. Mwegoha anasema mboga zilizomwagiwa
maji hayo zilibainika kuwa na sumu iliyotokana na madini ya risasi,
shaba na kromiamu ambazo zote zina madhara kwa binadamu.
Alisema utafiti huo ulihusisha wakulima
35 wa maeneo ya Jangwani, Kigogo, Vingunguti na Tabata Shule, ambao
wanatumia maji ya mto huo kumwagilia mboga za majani.
Dk. Mwegoha alisema katika utafiti huo
walibaini kuwa mboga hizo zinauzwa zaidi kwenye masoko ya Ilala,
Kariakoo, Buguruni, Vetenari, Tazara, Mwananyamala, Mnyamani, Kigogo,
Kisutu, Vingunguti, Tabata, Mikoroshini na maeneo ya jirani na wakulima
hao.
Pia anasema kwa mujibu wa utafiti huo, mboga hizo zinauzwa pia kwenye masoko ya maeneo mengine ya jijini humo.
Alisema licha ya Vingunguti kukuta bango
kubwa likitoa hadhari kwamba maji ya mto huo siyo salama kwa matumizi
ya binadamu, wanyama na kumwagilia mazao, bado wakulima walibainika
kuendelea kuyatumia.
Utafiti huo ulibaini kuwa asilimia 71 ya
wakulima wa mboga za majani wanatumia maji hayo na asilimia 63 hawajui
kama yana madhara na hayafai kumwagilia mazao, huku asilimia mbili
wakisema wanafahamu kuwa yana sumu.
Mhadhiri huyo anasema wakulima hao
wanapata kipato cha kuendesha maisha yao ambapo kwa wastani kwa mwezi
mmoja, mkulima anapata pato la kati ya Sh 89,000 hadi 300,000 kutokana
na biashara hiyo.
Licha ya kugundulika kuwa na sumu
inayotoka viwandani, maji mengine yanayotumika katika umwagiliaji wa
mboga hizo yamebainika kuchanganyika na majitaka yakiwamo yanayotoka
kwenye vyoo. Umwagiliaji huo unafanyika kuanzia kupanda mbegu hadi
uvunaji wa mboga.
Peter Mwakikao ni mmoja wa wananchi
wanaoishi Ubungo- Gereji, anasema kwa muda mrefu sasa mifereji ya maji
machafu imekuwa ikitiririsha maji kutoka viwandani kwenda kwenye
mashamba ya mboga za majani na makazi ya watu.
Licha ya matumizi ya maji hayo,
inaelezwa kuwa wakulima wa mboga wanatumia dawa za kukuzia na kuua
wadudu isivyostahili, hivyo kuzidi kuhatarisha afya za watumiaji wake.
Sehemu ya matumizi ya dawa hizo
inaelezwa kulenga kujinufaisha kujipatia kipato kwa kutumia madawa
yanayokuza mboga kwa muda mfupi.
WAKULIMA
Hata hivyo wakulima kadhaa wakiwamo wasiotaka majina yao kutajwa gazetini, wanataja ukosefu wa maji salama kwa umwagiliaji kuwa chanzo cha matumizi ya maji yasiyofaa kwa mimea na matumizi ya binadamu.
Hata hivyo wakulima kadhaa wakiwamo wasiotaka majina yao kutajwa gazetini, wanataja ukosefu wa maji salama kwa umwagiliaji kuwa chanzo cha matumizi ya maji yasiyofaa kwa mimea na matumizi ya binadamu.
“Hatuna namna nyingine zaidi ya kutumia
maji hayo… hakuna maji salama kwa umwagiliaji wa mboga hizi, na kwa vile
maisha yetu yanategemea rasilimali hii hatuwezi kuacha,” anasema mmoja
wa wakulima hao eneo la Keko Mwanga.
Anasema mbadala wa maji hayo ni wakati mvua zinaponyesha na si vinginevyo.
Naye Munga Mkude mkulima katika bonde la
Keko Mwanga, anasema ipo haja kwa serikali kuingilia kati na kubuni
miradi ya ujenzi wa visima virefu vitakavyo wawezesha kushiriki kilimo
cha umwagiliaji usiokuwa na madhara kwa mboga na afya za watu.
Kwa upande wake, mkulima Asumile
Mwakasala, anasema pamoja na kutumiwa na wananchi wa kawaida, mboga
wanazozilima zimekosa soko kwenye maduka makubwa maarufu kama Super
Markets.
Kutokana na ukosefu wa soko hilo,
wakulima hao wamewekeza zaidi kwa wafanyabiashara wanaonunua na kuziuza
kwenye masoko na makazi ya watu jijini humo.
Pamoja na hatari hiyo, wapo wakulima
akiwamo Lusako William wa Tabata Gereji waliochimba visima vipufi kwa
ajili ya kupata maji ya umwagiliaji mboga hizo.
Hata hivyo, NIPASHE ilipotembelea visima
hivyo ilibaini kuwa ni vifupi na maji yaliyomo ni yale yanayotoka
viwandani yakiwa na kemikali zenye sumu.
KAULI YA TFDA
Afisa uchanganuzi wa madhara yanayotokana na chakula katika Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Kaiza Kilango, anasema serikali inaendelea kukusanya mboga zinazouzwa kwenye masoko kadhaa jijini humo ili kuzipima.
Afisa uchanganuzi wa madhara yanayotokana na chakula katika Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Kaiza Kilango, anasema serikali inaendelea kukusanya mboga zinazouzwa kwenye masoko kadhaa jijini humo ili kuzipima.
Anasema hatua hiyo inalenga kubaini
ikiwa kuna mboga za majani zilizoathirika kwa kemikali ama kuwa na
vimelea vya magonjwa, hivyo kuwasiliana na maofisa kilimo wa halmashauri
husika.
“Huwa tunapita masokoni na tunanunua
bidhaa kama wateja wa kawaida, tukishazipima na kubaini zenye madhara
tunawataarifu wakurugenzi na maofisa kilimo ili wachukue hatua,” anasema
Kilango.
Anasema TFDA hawana uwezo wa kuwazuia
wakulima kumwagilia mboga kwa kutumia maji yenye kemikali zenye sumu ama
maji machafu kwa kuwa wajibu huo upo kwa mamlaka za halmashauri za
manispaa. Mbali na halmashauri za manispaa, Kilango, anasema taarifa za
ukaguzi huo zinawasilishwa kwa Baraza la Taifa la Hifadhi la Usimamizi
wa Mazingira (Nemc) ili kuchukua hatua dhidi ya kiwanda husika.
“Sisi tunaendelea na tutaendelea
kuelimisha watu hususani wakulima wenyewe wasitumie maji yanayotoka
viwandani kwa kuwa mara nyingi si salama kwa afya ya binadamu.” anasema.
0 Comments