Mfanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Patrick Pella amevamiwa na majambazi wenye silaha na kupigwa risasi, kujeruhiwa na kisha kuporwa fedha zake leo mchana maeneo ya Tabata-Relini jijini Dar es salaam
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, Pella anadaiwa kuporwa kiasi cha Sh. Mil 2
alizokuwa nazo akiwa ametoka kuzichukua kwenye mashine ya kutolea fedha
(ATM) Tawi la NMB liliyopo jirani na Azam TV, Barabara ya Mandela.
KWA TAARIFA ZAIDI BOFYA >>>
Mtandao
huu ulimtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Mary Nzuki kuelezea
zaidi tukio hilo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
via>> http://www.williammalecela.com
0 Comments