STAA mkongwe katika tasnia ya filamu, Blandina Chagula ‘Johari’
amefunguka kuwa kamwe hatarajii kuolewa na staa kama Vicent Kigosi ‘Ray’
bali anahitaji mume wa kawaida asiye maarufu. Akizungumza na Uwazi,
Johari alisema kuwa kwa upande wake hachagui mwanaume gani wa kumuoa
bali tu ajue kumthamini na kumuheshimu kama mwanamke......
Kwanza sihitaji mwanaume wa kunioa awe staa hata siku moja, nataka tu
awe wa kunijali na kunithamini na kingine awe mchapakazi kwa kuwa mimi
mwenyewe ni mtafutaji,” alisema Johari.
Awali, Johari aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nyota
wa filamu, Ray na kuachana baadaye. Kama ni hivyo basi mapenzi yao
yalikuwa ni ya ‘boyfriend’ na ‘girlfriend’ na wala si ndoa.
0 Comments