
Mwanza
ni moja ya sehemu tatu za Tanzania ambazo huwa nazipenda sana na hata
wakati mwingine kuvutiwa kuzitembelea kila ninapopata nafasi.
Mabadiliko ambayo wengi wangependa kuyaona ni jiji hili lilibarikiwa
kwa kupewa pia ziwa Victoria, liendelee kupendeza kihalali kutokana na
mpangilio unavyohitajika.

Hili
jengo linajengwa maeneo ya Capri Point ambapo ni jengo la Hoteli
litakalokuwa na gorofa kumi na tano, ni jengo la hoteli ambayo ni ya
Nyota tano itakayokuwa karibu na vyumba mia mbili vya kulala.

Limeanza
kujengwa tangu November 2013 na linatarajiwa kumalizika mwaka 2016 huku
gharama ya kulijenga ikiwa ni zaidi ya bilioni 72.
0 Comments