Ni
taarifa kutoka Dodoma ambapo tarehe 04.02.2015 askari Polisi Joseph
Isack Swai ameuwawa huku chanzo chenyewe kikielezewa kuanzia mwanzo
mpaka mwisho.
Alipigiwa simu na Mtendaji wa Mtaa wa chang’ombe juu Dodoma Mjini
akimjulisha kuwa amepokea taarifa ofisini kwake kutoka kwa OLIVER D/O
BALTAZARI, MIAKA 52, CHAGA, MKAZI WA CHANG’OMBE JUU kuwa kijana wake
aitwaye TISI S/O SIRILI MALYA ana mtesa mtOto wake mdogo wa miezi nane
aitwaye VALERIAN S/O TISI MALYA na anahisi labda ameshamuua kwani motto
huyo halii tena.
Polisi wamesema ‘alichofanya mtendaji ni kumpigia simu askari akaenda
wakaongozana pia na kijana mmoja hadi anakoishi huyo TISI S/O SIRILI
MALYA, walipofika askari aligonga mlango akijitambulisha kuwa yeye ni
askari hivyo atoke nje.
Swai wakati wa uhai wake.
Alichofanya mtuhumiwa huyo ni kumnyanyua mtoto wake mdogo wa miezi
nane kwa mkono mmoja miguu juu kichwa chini na kutaka kumkata kwa panga
na kusema ‘
namkata shingo na sitaki kuona mtu‘
Askari aliamua kumwokoa mtoto huyo na alipomrukia mtuhumiwa kwa
bahati mbaya aliteleza na kumkata kichwani askari na akadondoka chini
kutokana na jeraha kubwa ambapo hata hivyo mtuhumiwa aliendelea
kumkatakata ambapo Mtendaji na kijana waliyekuwa naye ambaye ni mratibu
wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu iliwabidi kukimbia huku na
kupiga kelele kuomba msaada.
Mtuhumiwa baada ya kufanya hicho kitendo alikimbia huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu akiwa na panga mkononi.
Askari
huyu muda mfupi kabla ya tukio hili alikuwa ametokea katika kituo cha
Redio cha Dodoma FM kwa ajili ya kuandaa kipindi cha kuielimisha jamii
juu ya ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) tunapoelekea
kipindi cha uchaguzi, kwani mbali na kazi anazofanya mojawapo ni
kushiriki katika vipindi vya kutoa elimu ya Polisi Jamii hapa mkoani
Dodoma.
Msako bado unaendelea ili kuweza kumtia nguvuni mtuhumiwa huyu
aliyesababisha kifo cha askari wetu wakati alipojitolea maisha ya ili
kumwokoa huyo mtoto mdogo.
Polisi wanasema ‘
tunazidi kuomba msaada
wa wananchi popote pale watakapomuona TISI S/O SIRILI MALYA, MIAKA 29,
MCHAGA ambaye ni maji ya kunde, mwembamba, siyo mrefu sana saizi ya kati
alikuwa amevaa suruali rangi ya blue iliyopauka na T-Shirt rangi ya
dark blue na kofia nyeupe yenye alama nyekundu ili tuweze kumkamata na
kumfikisha mahakamani.
Imetolea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi – Misime D.A (SACP)
0 Comments