Katibu
Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde (pichani), alitoa ahadi hiyo kama
zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpwapwa mkoani Dodoma,
kufuatia ajali ya moto iliyotokea Januari 20, mwaka huu na kuteketeza
mali zote zilizokuwa kwenye bweni la wasichana 64 wa kidato cha tano na
cha sita.
Dk.
Msonde alikuwa miongoni mwa viongozi walioongozana na Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi-Elimu), Kassim Majaliwa, kwenye ziara ya kutoa pole katika
shule hiyo.
“Zawadi
niliyowaandalia ni taarifa kwamba Februari 15, mwaka huu, tutatangaza
matokeo ya mitihani iliyofanywa na watahiniwa wa kidato cha nne nchini.
Nasema ni zawadi kwa sababu sijaitoa mahali kokote, nyie ndiyo wa kwanza
kuipata,” alieleza Msonde.
Watahiniwa
waliotarajiwa kufanya mtihani huo Novemba, mwaka jana ni 297,488 huku
watanihiwa 245,030 wakiwa wa shule na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa
52,448. Watahiniwa wa shule walioandikishwa ni wavulana 132,244
(asilimia 53.97) na wasichana 112,786 (asilimia 46.03).
Kupitia
ziara hiyo, Serikali imepeleka vitanda 64 ambapo magodoro 64 yalitolewa
na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene.
Pamoja
na misaada hiyo, aliahidi kupeleka madaftari, mikebe ya vifaa vya
hisabati, kalamu na kumpa kila mwanafunzi aliyekuwa akiishi kwenye bweni
lililoteketea fedha taslim ili anunue vifaa binafsi ambavyo
havikupatikana kwenye misaada iliyotolewa na wasamaria wema.
Aliongeza
kuwa shule hiyo itapelekewa vitabu vya aina zote kwa kiwango cha kila
mwanafunzi kuwa na kitabu chake, vitakavyonunuliwa kutokana na Sh.
bilioni 27 ambazo zimepatikana kutoka kwenye ‘chenji’ ya ununuzi wa
rada.
Pamoja
na misaada ya mahitaji binafsi ya wanafunzi inayopelekwa na watu
binafsi, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali, misaada mingine
inayoendelea kupelekwa ni vifaa vitakavyowezesha kujengwa kwa bweni
mbadala.
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (LAPF), umepeleka mabati 92 yenye thamani ya Sh. milioni mbili.
0 Comments