Jumla
ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya
mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la 10.08%
kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235227 sawa na 58.25
walifaulu.
Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo jijini Dar es
salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles
Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 89,845 sawa na asilimia
66.61 wakati wavulana ni 106,960.Amesema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167,643 sawa na asilimia
69.76 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 75,950 sawa na asilimia
68.70 na wavulana 91,693 sawa na asilimia 70.67.
Amesema mwaka 2013 watahiniwa 201,152 sawa na asilimia 57.09 ya
watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo hivyo ufaulu kwa wanafunzi wa
shule umepanda kwa asilimia 12.67 mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka
2013.
Akizungumzia ubora wa ufaulu, Dkt Msonde amesema kuwa jumla ya
watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na
Credit ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991 sawa
na asilimia 25.32 na wavulana ni 45,841 sawa na asilimia 35.33.
Watahiniwa waliopata daraja la PASS 93,811 sawa na asilimia 39.04 na
waliofeli kwa kupata daraja la FAIL 72,667 sawa na asilimia 30.24.
Kuhusu ufaulu wa masomo, Dkt Msonde amesema kuwa ufaulu katika masomo
ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22 ikilinganishwa na
mwaka 2013.
Ufaulu wa juu kabisa umekuwa katika somo la Kiswahili ambapo
asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wamefaulu na ufaulu chini kabisa ni wa
somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.58.
Amesema Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 184 baada ya kubainika
kufanya udanganyifu, kati yao 128 ni watahiniwa wa kujitegemea na 56 ni
watahiniwa wa shule.
BONYEZA MANENO HAYA KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2014
0 Comments