Mtu mmoja katika mahakama ya Kwale
nchini Kenya ameshtakiwa kwa kumkata pua na mkono mkewe ambaye anamshuku
kwa kufanya uasherati.
Kulingana na gazeti la the Nairobian
nchini Kenya,Chirope Mwaruwa anadaiwa kumkodisha mwanamume ili kulala na
mkewe mjamzito akidai kwamba ana matatizo.
Alishtakiwa kwa kumshambulia mkewe Sada Dzea katika kijiji cha Mukundi taarafa ya Mangawani ,kaunti ya Kwale.
Kulingana
na upande wa mashtaka Dzea mara ya kwanza alimkataa mtu aliyekodishwa
na mumewe wafanye naye tendo la ngono akiwa mjamzito.
Baada ya Dzea kukataa mumuwe alianza kumshtumu kwa kufanya uzinzi huku akitaka kumvua nguo kwa lengo la kutafuta ushahidi.
Na
alipokasirishwa na shtuma hizo Dzea alidaiwa kumtembelea mtu huyo
aliyekodishwa na mumewe ili afanye naye tendo la ngono kwa lengo la
kumfurahisha mumewe.
lakini kabla ya yeye kufika kwa mawanmume huyo mumewe mwenye wivu mwingi alidaiwa kumvamia na kuanza kumshambulia.
via>>BBC
0 Comments