Mara
nyingi watu huwa wanalalamika, wanasema viongozi na watu wenye pesa hata
wakifanya makosa hawafungwi, lakini ikitokea mtu wa kawaida kafanya
kosa lolote anahukumiwa kifungo, hapo ndio ambapo watu wanalalamikia
kwamba inaonekana kama hakuna usawa kwenye Sheria.
Mahakama ya Ivory Coast imemhukumu Simone Gbagbo mke wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo kifungo cha miaka 20 gerezani.
Simone amehukumiwa kifungo hicho baada ya
kukutwa na hatia ya kushiriki katika vurugu zilizotokea baada ya
uchaguzi nchini humo mwaka 2010 na 2011 na kusababisha vifo vya watu
zaidi ya elfu tatu.
Simone Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 pamoja na mume wake, Laurent Gbagbo ambaye
anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya
uhalifu ICC iliyopo The Hague, Uholanzi kwa makosa hayo kutokana na
machafuko yaliyotokea mwaka 2010 baada ya Rais huyo kugoma kukabidhi
madaraka kwa Alassane Ouattara aliyeshinda nafasi ya Urais kutoka chama cha upinzani.
0 Comments