Arsenal
imetinga nusu fainali ya kombe la FA baada ya kuitandika Manchester
united magoli 2-1 kwenye uwanja wa Old Trafford usiku wa kuamkia leo. Mchezaji wa zamani wa Man united Danny Welbeck aliifungia Arsenal bao la ushindi katika dakika ya 61.
Awali Arsenal ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 25 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wao Nacho Monreal na baadaye Man u kusawazisha dakika ya 29 kupitia kwa nahodha wao Wayne Rooney kabla ya Welbeck kuhitimisha ushindi.
Angel Di Maria alitolewa nje kwa kadi nyekundu dk77 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kumsukuma Michael Oliver.
0 Comments