Mchungaji wa kanisa analosali msanii wa filamu za Kibongo, Ruth Suka
‘Mainda’ na wenzake lililopo Sinza, Dar, Godwin Mwamposa amekanyaga
skendo kufuatia madai ya kumtelekeza mkewe aitwaye Sylvia mwenye mtoto
mmoja ambayo imetua kwenye dawati la gazeti hili.
Ndugu wa Sylvia afunguka
Awali,
ndugu aliyejitambulisha kuwa anaishi na Sylvia (jina tunalihifadhi kwa
sababu maalum) alisema mke wa mchungaji huyo kwa sasa anaishi maisha
magumu maeneo ya Buza jijini Dar baada ya kuachwa kwenye mataa na mwenza
wake huyo.
“Yaani mpaka nimeamua kuwaambia hii habari nimeona ndugu yangu anateseka
sana, tena na mtoto wake ambaye amekuwa akimuulizia baba yake kila
siku.
“Mgogoro ulianza siku nyingi wakiwa Moshi (Kilimanjaro) ambapo Mchungaji
Mwamposa alimwambia Sylvia wanakuja Dar kwa ajili ya kutoa huduma
lakini walipofika alimpeleka kwa wazazi wake Buza (Dar) na kumuacha
huko.“Kuna wakati wazazi wa Sylvia walimuita lakini alichenga kwenda,
hali iliyosababisha sintofahamu kwa wanandugu.
“Sylvia analia kila siku, mara ya mwisho alipata presha ya kushuka na
kulazwa Muhimbili (Hospitali ya Taifa) mpaka akawekewa mashine ya
kupumulia kwani alikuwa na hali mbaya lakini pamoja na hilo bado
mchungaji huyo hakusogea wala kuulizia hali yake,” alisema ndugu huyo.
Wakiwa na nyuso za furaha siku ya ndoa yao.
Ilidaiwa kwamba, kutokana na mazingira hayo, wanandoa hao waliofunga
ndoa mwaka 2008 huko Kilimanjaro kwenye Kanisa la Calvary Assemblies of
God, walikwenda kwenye usuluhishi katika makao makuu ya kanisa hilo
yaliyopo Morogoro lakini mambo hayakuweza kutengamaa.
Mke atafutwa
Baada
ya kupata habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Sylvia na kuzungumza
naye juu ya madai hayo ya kutelekezwa ambapo alikiri kuwepo tatizo
lakini akasema asingependa kuliongelea kwa sababu hakuwa na hali nzuri.
“Samahani sitaweza kulizungumzia sana suala hilo kwani sipo vizuri,” alisema Sylvia na kuomba apewe muda.
Mtoto
wa mchungaji naye anenaBaada ya kuzungumza na Sylvia, mtoto wa
mchungaji huyo aliyefahamika kwa jina la Angelprincess alizungumzia
mazingira magumu anayoishi kutokana na kuwa mbali na baba yake.
“Natamani kumuona baba yangu, naishi mazingira magumu na mama yangu.
Yaani siku nikimuona baba nitafurahi sana,” alisema mtoto huyo.Mchungaji
Mwamposa anasemaje?
Hii ni shahada ya ndoa yao.
Akizungumza
kwa njia ya simu na gazeti hili, mchungaji Mwamposa alionesha kuwapo
kwa tatizo kati yake na mkewe na akaeleza kuwa, suala lao lipo kwenye
uongozi wa juu wa kanisa lake.
“Kama
mnaweza kumsaidia msaidieni lakini suala hili lipo kwa uongozi wa juu
wa kanisa na mkitaka zaidi mtafuteni wakili wangu muongee naye.”
Licha
ya kiongozi huyo wa dini kumpatia mwandishi namba ya simu anayotumia
mwanasheria huyo, ilipopigwa iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na
hata alipotumiwa meseji hakujibu hadi tunakwenda mtamboni.
Gazeti hili linaendelea kufuatilia habari hii kwa karibu na chochote kitakachopatikana, utakisoma kwenye Magazeti ya Global.
0 Comments