STAA wa
filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibu alijikuta akimwaga machozi baada
ya kutembelea shule ya watoto wenye ulemavu ya Salvition Army, iliyopo
Kurasini jijini Dar.
Staa huyo akiwa na timu yake ya Rozzie Magazine, walibeba misaada
mbalimbali ikiwemo mchele, mafuta, maharage na sukari ambapo mara baada
ya kufika kwenye ukumbi maalum uliotaarishwa kwa ajili ya kuzungumza na
watoto hao, alishikwa na moyo wa huruma na kudondosha machozi.
“Kuna kitu nimejifunza hata kama hatuna tunahitaji kuja kuonana na
watoto hawa kuzungumza nao na kuwafariji hivyo hata wasanii wenzangu
wanapaswa kufanya hivi kwani ni muhimu katika maisha yetu,” alisema
Rose.
0 Comments