‘Leo Tena‘ ya Clouds FM ilipata nafasi ya kumuuliza swali hili Tunda Man kwamba ikitokea akaambiwa aurudie wimbo wa msanii wa Tanzania atakua tayari kurudia wimbo gani na kwa sababu gani.
Wimbo wa kwanza ambao Tunda Man kautaja ni ‘Mkasa wa Bosi‘, wimbo ambao umeimbwa na Ferooz na wimbo wa pili alioutaja ni wimbo wa ‘Kamanda’ ambao umeimbwa na Daz Nundaz.
Tunda Man
alisema ametamani kuzifanya upya nyimbo hizo lakini akitafuta kisa cha
kubadilisha haoni na kwake yeye anaona ni nyimbo za ajabu sana kiasi cha
kutamani kuzirudia kwa mashairi hayo hayo ila kwa namna nyingine.
0 Comments