![]() | |
| Miongoni mwa nyumba zilizobomolewa katika tukio hilo |
Watu 38 wamefariki dunia
na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na
mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo
katika kijiji cha Mwakata Kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.
Akiwa eneo la tukio, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema waliokufa wengi ni watoto ambao walisombwa na maji baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao na kwamba majeruhi walelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
![]() |
| miti ikiwa imeny'oka baada ya mvua hiyo |
![]() |
| mkuu wa wilaya ya kahama na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo akiongea na wananchi na eneo hilo |
![]() |
| mchungaji akitoa sala fupi kwa tayari kuwahifadhi ndugu zetu waliopoteza maisha |
Amesema majina ya waliokufa kwa sasa bado hayajatambulika na kwamba kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa wa shinyanga inakaa jioni hii ili
kutathimini maafa hayo pamoja na kujua ni msaada gani unahitajika kwa
wahanga hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada.
Akiwa eneo la tukio
Mpesya ametoa agizo kwa uongozi Redcross na jeshi la Scauti kuhakikisha
wanasaidia katika familia zilizokutwa na maafa hayo wakati serikali
ikisubiri kukamilika kwa zoezi la sense ya wahanga hao aliloagiza
kufanywa na viongozi wa eneo hilo.
Dunia kiganjani blog imefika katika eneo la tukioa na kushudia nyumba za kaya mbalimbali katika kijiji hicho zikiwa zimebomoka na nyingine kuezuliwa mapaa huku hali ya mazao na miti ikiharibiwa vibaya na mvua hiyo ambayo pia imeuwa mifugo.





0 Comments